17 Juni 2026 - 13:54
Rais Pezeshkian: Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kwa Mahujaji Uliweka Alama Muhimu katika Hija ya Mwaka Huu

Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amesema ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa mahujaji wa Kiislamu umeifanya Hijja ya mwaka huu kuwa ya kipekee, huku akiwapongeza viongozi na watendaji wa Hijja kwa kuhakikisha mahujaji wa Iran wanatekeleza ibada zao kwa usalama, afya njema na heshima.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (AS) –ABNA– Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, amesema kuwa ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu uliotolewa kwa mahujaji wa Kiislamu umeacha athari kubwa na kuwa hatua muhimu iliyotofautisha msimu wa Hijja wa mwaka huu.

Katika ujumbe alioutoa kufuatia kurejea salama kwa mahujaji wote wa Iran nchini, Rais Pezeshkian alieleza kuwa uamuzi wa Kiongozi wa Mapinduzi wa kusisitiza kutekelezwa kwa ibada ya Hijja, pamoja na ujumbe wake wenye maudhui ya kina uliowaelekeza Waislamu wote walioshiriki mkutano mkubwa wa Hijjah, uliifanya Hijja ya mwaka huu kuwa na umuhimu wa kipekee.

Rais huyo pia alitoa shukrani kwa Waziri wa Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu, Abbas Salehi, mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi na mkuu wa ujumbe wa mahujaji wa Iran, Mkuu wa Shirika la Hijjah na Ziara, pamoja na watendaji wote waliohusika na huduma za Hijja kwa juhudi zao katika msimu wa mwaka huu.

Aidha, aliwapongeza wote waliohusika kwa huduma walizowapatia mahujaji wa Iran katika Ardhi Takatifu licha ya changamoto zilizokuwepo, akisisitiza kuwa juhudi hizo ziliwawezesha mahujaji kutekeleza ibada zao kwa afya njema, usalama na heshima.

Rais Pezeshkian alihitimisha kwa kusisitiza kuwa msimamo wa Kiongozi wa Mapinduzi kuhusu Hijja na ujumbe wake kwa Waislamu wa dunia uliweka alama ya kihistoria na kuwa mojawapo ya matukio muhimu zaidi katika msimu wa Hijja wa mwaka huu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha